WHO: Algeria, Argentina zimetokomeza Malaria

WHO inasema Algeria na Argentina zimefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa Malaria. Picha na AFP

Spread the love

Shirika la afya duniani (WHO) linasema mataifa ya Algeria na Argentina yamefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa Malaria.

Hatua hii inamaanisha katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, hakujaripotiwa hata kisa kimoja cha mgonjwa wa malaria katika nchi hizo.

Malaria ugonjwa unatokana na kuumwa na mbu umesalia kuwa ni moja ya magonjwa yanayoongoza kwa vifo duniani.

Inakadiriwa kuwa mwaka 2017 pekee watu zaidi ya laki nane duniani kote walipoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Malaria, asilimia 60 ya vifo hivyoikiwa ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Algeria ni nchi ya pili katika ukanda wa Afrika wa WHO kutambuliwa rasmi kama imetokomeza malaria baada ya Mauritius ambayo ilithibitishwa rasmi mwaka  1973.

WHO inasema Algeria na Argentina zimefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa Malaria. Picha na AFP

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *