Mwili wa Ettiene Tshisekedi kurejeshwa DRC kwa maziko

Kinara wa upinzani wa muda mrefu nchini DRC aliyeaga dunia mwaka 2017 na anatarajiwa kuzikwa mwezi Juni. Picha na AFP

Spread the love

Mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Ettiene Tshisekedi unatazamiwa kurejeshwa nchini DRC Mei 30 na kuzikwa Juni 1 katika viunga vya jiji la Kinshasa.

Kiongozi huyo aliaga dunia mapema mwaka 2007wakati akipatiwa matibabu Mjini Brussels nchini Ubelgiji.

Tangu hapo mwili wake haukurejeshwa nchini DRC kutokana na mvutano uliokuwepo baina ya serikali ya rais Joseph Kabila na wapinzani.

Hadi kufariki kwake, alikuwa kiongozi wa muda mrefu wa upinzani, akiongoza chama cha UDPS laini aliwahi kuhudumu kama Waziri Mkuu wakati wa utawala wa rais wa zamani Mobutu Seseko mwaka 1991,1992-1993 na baadaye 1997.

Tshisekedi alihudumu kwa miaka mingi kama kiongozi wa upinzani na aliyeheshimika na raia wengi wa Congo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *