Unalifahamu Jimbo la Kano nchini Nigeria

Chuo Kikuu cha Kano, ni mojawapo ya taasisi za elimu zinazopatikana katika Jimbo la Kano

Spread the love

Jimbo la Kano ni mojawapo ya majimbo 36 yanayounda taifa la Nigeria, likipatikana kaskazini mwa Nigeria. Mji Mkuu wa Jimbo hilo upo katika Mji wa Kano.

Jimbo hilo linapakana na majimbo ya Katsina lililopo kaskazini magharibi, Jimbo la Jigawa lililopo kaskazini mashariki, Jimbo la Bauchi lililopo Kusini mashariki na Jimbo la Kano lililopo kusini magharibi.

Lugha inayozungumzwa na wakazi wengi wa Jimbo hili ni Kihausa ingawa kuna wazungumzaji wachache wa lugha ya Fulani.

Jimbo la Kano lina vyuo vikuu vinne kikiwemo Bayero na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kano. Pia kuna vyuo vya kati zaidi ya 10 na kuwa miongoni mwa majimbo yenye taasisi nyingi za elimu nchini Nigeria.

Tovuti na jarida la Forbes Magazine (www.forbes.com) limewahi kuarifu kuwa tajiri namba moja barani Afrika Aliko Dangote mwenye utajiri wa dola za Marekani bilioni 10.6 ni mzaliwa wa Jimbo la Kano

Mji wa Kanoni makao makuu ya Jimbo la Kano lililopo Kaskazini mwa Nigeria.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *