Aristide Bance, mchezaji raia wa Burkinafaso aliyeweka rekodi kwa kucheza timu 22

Aristice Bance, mchezaji wa safu ya ushambuliaji wa kimataifa wa Burkinafaso. Picha kwa hisani ya mtandao wa goal.com

Spread the love

Mashabiki wa soka Tanzania, jina Aristice Bance sio geni masikioni mwao kwakuwa mwaka juzi mchezaji huyo raia wa burkina Faso alikuja nchini humo akiwa na klabu ya Al Masry ya Misri kucheza mechi ya kombe la shirikisho dhidi ya Simba.

Basi ripoti mpya zikufikie kuwa Bance amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Horoya ya Guinea akitokea klabu ya USFA inayomilikiwa na jeshi la Burkinafaso, aliyokuwa akiitumikia kwa mkopo.

Horoya inakuwa klabu ya 22 kuichezea katika maisha yake ya soka, huenda akaingizwa kwenye kumbukumbu kama miongoni mwa wachezaji waliocheza klabu nyingi duniani.

Mataifa mengine ambako alicheza soka ni Latvia, Ujerumani, Finland, Falme za Kiarabu, Ivory Coast, Ubelgiji, Misri, Ukraine, Watar, Afrika Kuisni, Uturuki na Kazakhstan.

Timu ya Taifa ya Burkinabe ameitumikia mara 74 akifunga mabao 22 na ameshiriki fainali tatu za kombe la mataifa ya Afrikam mwaka 2013, 2015 na 2017.

Je wachezaji wa Afrika Mashariki wanaweza kudumu kwa miaka mingi katika mchezo wa soka?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *