Mambo 10 unayopaswa kuyaona, kuyafanya uwapo Mji Mkongwe

Eneo la Ngome Kongwe kama linavyoonekana Mjini Zanzibar. Picha kwa hisani ya Mtandao wa zanzibar24.co.tz

Spread the love

Mji Mkongwe au kwa Kimombo Stone Town ni mojawapo ya maeneo ya yanayounda mamlaka ya Mji wa Zanzibar na Mji huu unatambuliwa kwa majengo mbalimbali ya kale yaliyojengwa miaka ya zamani.

Mwaka 2000 Mji Mkongwe au Stone Town ulitambuliwa rasmi kuwa urithi wa dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia elimu na sayansi, UNESCO.

Mji huo unajulikana kwa urithi wa kitamaduni wa kiarabu, India, Persia na Ulaya.

Mtandao wa culturetrip.com umeorodhesha maeneo kumi ambayo ufikapo Zanzibar hupaswi kutoyafikia au kukosa kuyaona uwapo katika mji huo.

Maeneo hayo ni Bustani ya Forodhani, sehemu ambapo mamia kwa maelfu ya wazanzibar hufurika kwa mapumziko.

Ngome Kongwe ni jengo la kale lililojengwa na waarabu kunako karne ya 17. Lilijengwa kwa lengo la kujilinda na uvamizi wa Mreno.

Soko la Darajani, eneo lingine maarufu katika Mji Mkongwe, ukitaka kutazama uzuri wa Afrika amshariki tembelea soko la darajani lililopo maili chache kutoka bandari ya Malindi.

Kanisa Anglikana la Mkunazini, kanisa hilo lilijengwa mwaka 1873 na Edward Steere, Askofu wa tatu wa Zanzibar. Kwa sasa linatumika kama kanisa Kuu la Kianglikana (Anglican Cathedral). Upeke wa kanisa hilo ni kwa nanmna lilivyojengwa likiambatanishwa na kichoro mbalimbali, pia mahala hapa palijengwa eneo la kuuzia watumwa kwenda mashariki ya mbali.

Kisiwa cha Changuu, kinapatikana karibu dakika 20 kwa barabara kutoka Mjini kati na kisiwa hiki ni makazi ya kombe ambao wengine wanakadiriwa kuwa na umi wa miaka 200 na bichi za kisasa. Pia inaelezwa kuwa kisiwa hiki kilitumika kuhifadhi wafungwa.

Msikiti wa Malindi, ni msikiti wa kale na ili kuutazama huna budi kusimama katika mabaraza yaliyopo pembezoni mwa mji huo.

Kanisa la Mtakatifu Joseph. Ni kanisa katoliki lililojengwa mwaka 1893 hadi 1897 na wamishenari wa kifaransa kwa mtindo wa kiromani. Wataalamu wa jengo hilo walitoka katika Mji wa Marseilles nchini Ufaransa.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *