Ufahamu Mji wa Kilwa uliotambuliwa kuwa urithi wa dunia 1981

Msikiti uliojengwa karne ya 12, unapatikana Kilwa Kissiwani. Picha kwa hisani ya mtandao wa Kilwa Tourism

Spread the love

Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayotajwa kubarikiwa na idadi ya vivutio vingi vya utalii duniani.

Mojawapo ya vivutio hivyo ni Mji wa Kilwa au Kilwa kisiwani uliopo kilomita 250 kutoka Jiji kuu la kibiashara la Dar es Salaam.

Kuanzia karne ya 11 mpaka karne ya 16 Mji huu ulikuwa kitovu cha shughuli za kibiashara katika ukanda wa bahari ya Hindi, kwa mujibu wa mtandao wa easy travel

Mji wa Kilwa umegawanyika katika maeneo makuu matatu, Kilwa Kisiwani, Kilwa Kivinje na Kilwa Masoko. Kilwa Masoko ni mji ulioendelezwa kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu ilhali miji ya Kilwa Kivinje na Kilwa Kisawani imejikita zaidi katika shughuli za utalii.

Mji wa Kilwa Kisiwani umapmbwa na Msikiti uliojengwa karne ya 12 na mapango mbalimbali ambayo yanaashiria uwepo wa wareno katika pwani ya Afrika mashariki.

Kilwa Kivinje, ni mji uliokuwa na shughuli nyingi enzi za kale ikiwemo ununuzi wa pembe za nduvu na shughuli ya ununuzi na uuzaji wa watumwa kwenda mashariki ya mbali. Wajerumani walipoitawala Tanganyika waliubadilisha mji huu kwa kuuendeleza zaidi na kuwa mji wa kisasa.

Je unataka kuufahamu zaidi mji wa Kilwa, tafadhali tembela tovuti yetu mara kwa mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *