Ufaransa yaongoza kwa kutembelewa na watalii wengi duniani

Mnara wa Eiffel uliopo Jijini Paris ambapo watu wengi hupoenda kujipumzisha hususani ni kipindi cha kiangazi. Picha kwa hisani ya tovuti ya mtandao wa france-justforyou.com

Spread the love

Nchi ya Ufaransa imeshika nafasi ya kwanza kwa kutembelewa na idadi kubwa ya watalii duniani mwaka 2018, ripoti ya tovuti ya mtandao wa France Just For You imebainisha.

Kwa mujibu wa takwimu hizo mwaka 2018 pekee taifa hilo lilitembelewa na idadi ya watalii milioni 89.4.

Hispania imeshika nafasi ya pili kwa kutembelewa na watalii milioni themanini na mbili na Marekani, taifa kubwa kwa nguvu za kiuchumi na kijeshi duniani lilitembelewa na watalii milioni sabini na nane.

Moja ya sababu zilizofanya Ufaransa kutembelea na idadi kubwa ya watalii ni Mji wa Paris, unaotajwa kuwa miongoni mwa majiji bora duniani, ukiwa na maje go ya kale yaliyonakshiwa kwa aina ya urembo. Pia Mnara wa Eiffel, uliopo katikati mwa jiji la Paris unatajwa kuvutia idadi kubwa ya watu kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Aidha jengo la kanisa la kikatoliki la Notre Damme, lililojengwa miaka zaidi ya 1200 iliyopita huvutia mamilioni ya watu kila mwaka.

Pia uwepo wa maeneo 44 yanayotambuliwa na shirika la elimu na sayansi la Umoja wa Mataifa UNESCO kama urithi wa dunia, mfano wa maeneo haya ni milima ya Alps,

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *