Upekee wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saa Nane

anafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino walipotembelea Kisiwa cha Saanane mwaka 2015. Picha na Maktaba ya Tanzania Reports

Spread the love

Kisiwa cha Saa Nane kinapatikana kusini mwa Mji wa Mwanza. Kihistoria eneo hilo lilikuwa likikaliwa na Mzee Saanane Chamwandi, mvuvi mashuhuri ambaye baadaye aligeukia kazi ya ukulima. Baadaye mzee huyo alilipwa fidia ili kupisha eneo hilo ambalo lilianza kumilikiwa na serikali ya Tanzania mwaka 1964.

Mamlaka za Tanzania zinazosimamia sekta utalii mwaka 2013 zilipandishwa hadhi, Kisiwa cha Saa Nane kuwa hifadhi ya Taifa.

Kisiwa hicho kina ukubwa wa kilomita za mraba 2.18 na kinaundwa na visiwa vidogo vitatu vyenye manzari ya kuvutia kwa wakazi wa jiji hilo.

Ni hifadhi yaa kwanza kupatikana ndani ya jiji na pia ni hifadhi ndogo ya wanyama katika eneo lote la Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla, mtandao wa utalii Tanzania umearifu (www.tanzaniatourism.go.tz).

Wanyama waliopo katika hifadhi hiyo ni swala, pundamilia, mamba, mijusi, nyoka na ndege wa aina mbalimbali.

Licha ya kutokuwa na idadi kubwa ya watalii ikilinganishwa na maeneo mengi ya nchi hiyo, ksiiwa hichohutembelea na wanafunzi wa vyuombalimbali vilivyopo Mkoani Mwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *