Antonio Gutteres, Katibu Mkuu wa tisa wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutteres akiwa ziarani nchini Fiji hivi karibuni. Picha na Umoja wa Mataifa

Spread the love

Umoja wa Mataifa (UN) ni taasisi nambari moja duniani inayoratibu shughuli za kidiploamsia. Taasisi hii iliundwa April 25 mwaka 1945 kwa lengo la kuwaleta pamoja viongozi wa dunia na kushirikiana katika malengo ya pamoja na kustawisha amani na usalama duniani.

Wakati wa kuundwa kwake UN ilikuwa na wanachama waanzilishi 51 na kufikia sasa ina wanachama 193.

Ili kufanikisha uendeshaji wake Umoja wa mataifa unaundwa na vyombo mbalimbali ikiwemo baraza la usalama la Umoja wa mataifa, mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa, baraza la haki za binadamu, sekretarieti n.k.

Taasisi hii kwa sasa inaongozwa na Antonio Gutteres ambaye ni katibu mkuu wa tisa, akitanguliwa na makatibu wengine wanane ambao waliwahi kuhudumu katika taasisi hiyo.

Gutteres ni mwanadiplomasia na mwanasiasa raia wa Ureno ambaye kabla ya kushika madaraka ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2017, alikuwa kamishna wa shirika la wakimbizi la Umoja huo kwa miaka kumi (2005 hadi 2015)

Katika maisha yake kisiasa nchini Ureno, alihudumu katika nafasi ya Waziri mkuu kwa miaka saba (1997-2002) na katibu mkuu wa chama cha kisoshalisti kwa miaka kumi.

Kura ya maoni iliyopigwa nchini mwake kutoka 2012 hadi 2014 ilimtaja Gutteres kuwa waziri mkuu bora wa Ureno katika kipindi cha miaka 30.

Mwaka 2018, kufuatia mazungumzo baina ya Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, Gutteres aliitaja hatua hiyo kama ya kihistoria na inayoweka msingi wa kuondokana na silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.

Kwa mujibu wa kituo cha CNN, Gutteres ni muumini wa dini ya kikristo wa madhehebu ya katoliki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *