Kwanini dunia inaadhimisha siku ya redio?

Maadhimisho ya siku ya radio kimataifa 2013 katika makao makuu ya UNESCO yaliyopo Paris Ufaransa. Picha na Wikipedia

Spread the love

Kila mwaka ifikapo February 13 dunia huadhimisha siku ya kimataifa ya redio kwa kihispaniola ikifahamika kama Dia Mundial De La Redio iliidhinishwa rasmi na shirika la sayansi na elimu la Umoja wa Mataifa UNESCO katika mkutano wa 36 uliofanyika nchini Hispania.

Ukweli ni kwamba radio katika karne ya 21 imemsalia kuwa chombo muhimu cha kupashana habari na kuwafikia mamilioni ya watu wengi ulimwenguni hususani wanaoishi maeneo ya vijijini.

Septemba 29 bodi ya UNESCO kwa ushawishi wa Hispania ilikubaliana na ombi la Uhispania la kuadhimisha siku ya kimataifa ya radio.

Bodi ya UNESCO baada ya kukubaliana na pendekezo la Hispania ilifanya mashauriano na wadau mbalimbali wa sekta ya habari na utangazaji yakiwemo mashirika makubwa ya habari kama Shirika la Jtangazaji la Mataifa ya Kiarabu (ASBU), North America Broadcasting Association (NABA), Muungano wa Utangazaji wa Ulaya (EBU) na mengine.

Mwaka 2012 mkutano wa Umoja wa Mataifa uliidhinisha rasmi uwepo wa siku ya kimataifa ya Radio File kupitia azimio namba A/RES/67/124

Mwaka 2019 siku hiyo iliadhimishwa kwa kauli mbiu ya majadiliano, uvumilivu na amani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *