Johanna Konta afuzu robo fainali ya michuano ya tenisi ya Ufaransa

Johanna Konta amefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya tenisi ya Ufaransa.

Spread the love

Mchezaji wa tenisi namba moja nchini Uingereza Johana Konta amefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Tenisi ya Ufaransa, French Open kwa mara ya kwanza akimshinda mchezaji namba 23 kwa ubora duniani kutoka Croatia Donna Vekic.

Konta ameshinda kwa seti mbili za 6-2 6-4 na sasa Konta anatumai kufika hatua ya nusu fainali ambayo kwa mara ya mwisho ilifikiwa na mwingereza mwenzie Jo Durie aliyefika hatua hiyo katika michuano ya French Op[en mwaka 1983.

Katika hatua ya robo fainali Konta atachuana na mshindi wa taji hilo mwaka 2016 Garbine Muguruza au mshindi wa mbili mwaka jana Sloane Stephens.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *