Mbuga ya wanyama ya Serengeti yashinda tuzo ya hifadhi bora Afrika

Mbuga ya wanyama ya Serengeti iliyopo nchini Tanzania. Picha kwa hisani ya tovuti ya www.serengetinationalpark.com

Spread the love

Mbuga ya wanyama ya Serengeti iliyopo kaskazini magharibi mwa tanzania imeibuka mshindi wa mbuga bora ya wanyama Afrika.

Tuzo hizo zimefanyika nmchini Mauritius na kuandaliwa na taasisi ya Worlk Travel Awards iliyoasisiwa mwaka 1993 ili kutambua ubora wa vivutio vya kitalii sehemu mbalimbali barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Hii ni mara ya pili kwa Serengeti kuibuka kinara ambapo mwaka jana katika tuzo hizohizo ilitajwa kuwa bora ya wanyama.

Milima ya Table iliyopo Afrika Kusini imeongoza kwa kuwa kivutio kinachoongoza barani Afrika kuvutia watalii wengi.

Jiji la Nairobio limetajwa kuwa jiji bora barani Afrika na kuwa kivutio kwa watu wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *