Bosi wa CAF akamatwa nchini Ufaransa

Bosi wa shirikisho la kandanda barani Afrika, Ahmad Ahmad.

Spread the love

Rais wa Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF Ahmad Ahmad ameshikwa na vyombo vya usalama nchini Ufaransa kwa tuhuma za rushwa.

Jarida la kila wiki la michezo nchini Ufaransa la Jeune Afrique limeripoti kushikiliwa kwa kiongozi huyo wakati akihudhuria mkutano wa Fifa nchini humo.

Inaelezwa kuwa kiongozi huyo amekamatwa akihusishwa na tuhuma za rushwa wakati CAF ikiingia mkataba na kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma ya Ujerumani.

Inaelezwa kampuni hiyo ililipa kiasi cha Euro 739 000 kwa Ahmad Ahmad ili kupata mkataba huo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *