KQ yasitisha safari za kwenda na kutoka Sudan

Shirika la ndege la ndege la Kenya limesitisha safari zake za kwenda na kutoka nchini Sudan

Spread the love

Shirika la ndege la Kenya Kenya Airways limesitisha safari zake za kwenda na kutoka nchini Sudan kutokana na hali ya kiusalama.

Sudan inashuhudia hali tete ya kiusalama na kisiasa huku vikoso vya serikali vikiendesha mauaji ya waandamanaji wanaopinga serikali ya kijeshi.

Katika taarifa yake shirika hilo limesema linatathimini hali ya mambo inayoendelea Sudan kabla ya kurejea kwa safari zake.

Kwa mujibu wa madaktari, wanasema watu zaidi ya 100 wameuawa lakini wizara ya afya inasema ni watu 46 pekee waliopoteza maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *