Mechi ya Esperance na Wydad kurudiwa, Esperance wapinga

Kikosi cha Esperance ya Tunisia

Spread the love

Wakati shirikisho la kandanda barani Afrika CAFlikitangaza kurudiwa kwa mchezo wa pili wa fainali ya klabu bingwa Afrika baina ya Esperance ya Tunisia na Wydad Casablanca ya Morocco, Esperance imepinga mpango huo.

Azimio la kurudiwa kwa mchezo huo lilifikiwa wakati wa kikao cha kamati ya utendaji ya CAF kilichoketi Paris, Ufaransa ambapo sasa mchezo huo utarudiwa baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Hata hivyo, Esperance imepinga hatua hiyo na kusema itakata rufaa katika mahaka ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo CAF.

Awali Esperance ilikabidhiwa ubingwa baada ya wapinzani wao kugomea kuendelea na mchezo wakipinga hatua ya mwamuzi Papa Bakary Gasama kulikataa bao la kusawazisha walilodai lilikuwa halali licha ya kuombwa atazame marejeo ya teknolojia ya video VAR.

Mchezo huo ulivunjika dakika ya 62 na licha ya jitihada za maofisa wa timu zote mbili kuwasihi wachezaji wa Wydad krejea mchezoni lakini hazikufanikiwa.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *