Neymar kukosa michuano ya Copa America

Mchezaji wa Brazail Neymar akitolewa uwanjani baada ya kuumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil. Picha na AFP

Spread the love

Mshambuliaji nyota wa Brazil, Neymar atakosa michuano ya mataifa ya Amerika Kusini maarufu kwa jina la Copa America.

Mchezaji huyo  aliumia kifundo cha mguu katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya Brazil na Qatar ambao Brazil ilishinda mabao 2-0.

Nyota huyo anayeitumikia PSG ya Ufaransa alitol;ewa uwanjani dakika ya 17 ya mchezo.

Michuano hiyo inayoshirikisha timu 12 itaanza Juni 14 na hii itakuwa mara ya kwanza kwa Neymar kukosa kuitumikia Brazil tangu alipovuliwa kitambaa cha unahodha mwezi Mei.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *