Samatta ageuka lulu, Uingereza

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta. Picha kwa hisani ya Mtandao wa Goal

Spread the love

Klabu za soka za Burnley, Brighton, Aston Villa na Leceister City za England zimeingia katika vita ya kuwania saini ya mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Samatta wa Tanzania

Samatta kwa sasa anaitumikia klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ambayo msimu uliomalizika ameiongoza kushinda taji la ligi kuu ya Ubelgiji akiwa mfungaji bora kwa mabao 23.

Gazeti la The Sun la Uingereza limesema Samatta ambye amebeba mikoba ya unahodha kuiongoza Timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars katika michuano ya AFCOBN huko Misri anatajwa kuwa na thamani ya paundi millioni 12,

Samatta mwenye umri wa mika 26 ndiye nguzo ya kuivusha Taifa stars katika michuano hiyo.

Kwa sasa Samatta yuko kwenye kmabi ya timu ya taifa ya Tanzania ambayo inajiandaa kucheza fainali za mataifa Afrika zinazotazamiwa kuanza baadaye mwezi huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *