WHO: Mtu mmoja kati ya wanne, hawafahamu wameambukizwa Ebola nchini DRC

Mazishi ya mtu aliyefariki duniani baada ya kuambukizwa na ugonjwa hatari wa Ebola REUTERS/Baz Ratner

Spread the love

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa mtu mmoja kati ya wanne Mashariki mwa DRC, ameambukizwa ugonjwa hatari wa Ebola lakini hafahamu.

WHO imetoa imesema hilo wakati huu inapoendelea kusaidia kupambana na maambukizi ya Ebola hasa mjini Beni, ambapo watu zaidi ya 2,000 wameambukizwa na wengine 1,357 wamepoteza maisha tangu mwezi Agosti mwaka 2018.

Siku za hivi karibuni, Wizara hiyo inasema maafisa wa afya wamejitahidi kutoa taarifa kuhusu namna ya kujizuia kupata ugonjwa huo, lakini watalaam wanaonya kuwa ni muhimu sana kuwepo kwa uangalifu mkubwa.

Visa vya maafisa na vituo vya afya kushambuliwa, pia vimepungua ikilinganishwa na miezi iliyopita.

Ugonjwa wa Ebola uligundulika katika Jimbo la Kivu Kaskazini tarehe 1 mwezi Agosti mwaka 2018 na ukasambaa katika hadi Ituri, lakini haujasambaa katika mataifa jirani.

Hii ni mara ya 10 kwa Ebola kuikumba nchi ya DRC, mara ya kwanza ikiwa mwaka 1976 na maambukizi haya ni mabaya baada ya yale yaliyoshuhudiwa katika nchi za Afrika Magharibi kati ya mwaka 2014-2016 na kusababisha vifo vya watu 11,300 hasa nchini Sierra Leone.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *