Dag Hammarskjöldm katibu mkuu wa UN aliyepoteza maisha kwa ajali ya ndege

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld

Spread the love

Matukio ya ajali ya ndege yaliyoua viongozi mashuhuri duniani si mageni, Juvenali Habyarimana rais wa Rwanda alipoteza maisha baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kigali kudunguliwa wakati ikijiandaa kutua katika uwanja wa ndege wa Kigali.

Profesa George Saitoti ni mwanasiasa mwingine mashuhufri kuwahi kutokea nchini Kenya na aliuawa mwaka 2013 baada ya ndege ndogo aliyokuwa akisafiria kupoteza uelekea na kuanguka nchini Kenya.

Dag Hammarskjöldm alikuwa katibu mkuu wa pili wa Umoja wa Mataifa na alipoteza maisha mwaka 1961 baada ya kuanguka kwa ndege aliyokuwa akisafiria DC-6 katika Mji wa Ndola. Yeye na watu wengine 15 wote walipoteza maisha katika ajali hiyo ambayo inatajwa kuwa mojawapo ya matukio mabaya kutokea kwa wanadiploamasia.

Alikuwea akielekea nchini Kongo kusuluhisha mgogoro nulitokana na kulipuka kwa mapigano baina ya vikosi vya serikali ya Kongo vikiongoza na Moise Tshombe na vile vya umoja wa mataifa.

Uchunguzi kuhusu kifo chake umechukua muda mrefu huklu baadhi ya ripoti zilizochapishwa katika filamu ya Cold Case Hammarskjöld zikiwafichua baadhi ya watu muhimu waliohusika katika mauaji ya kiongozi huyo.

Aidha mwaka 2015 aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban-Ki Moon aliunda tume ya kuchunguza mauaji ya kiongozi huyo ambayo iliwahusisha watu mashuhuri duniani akiwemo aliyekuwa jaji Mkuu wa Tanzania, Chande Othman.

Je nani alihusika na mauaji ya Dag Hammarskjöldm? Ni swali ambalo bado majibu yake hayajapatikana bayana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *