UNICEF:Watoto milioni 115 wa kiume walioa wakiwa watoto

Barubaru katika manispaa ya Gujara kwenye jimbo la Rautahat nchini Nepal wakiwa katika mchezo wa kuigiza wa ndoa za umri mdogo ulioandaliwa na UNFPA na UNICEF

Spread the love

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF inasema watoto wavulana na wa kiume milioni 115 walioa wakiwa watoto.

Ripoti hiyo ya kwanza kabisa ya aina yake kuhusu watoto inaonesha kuwa wavulana walioa wakiwa na umri mdogo na kwamba mtoto mmoja kati ya watano alioa kabla ya kutimiza umri wa miaka 15.

Ripoti hiyo iliyokusanya takwimu kutoka nchi 82 inatanabaisha kwamba ndoa za utotoni miongoni mwa watoto wa kiume zimekita mizizi katika nchi nyingi kote ulimwenguni kuanzia kusini mwa Jangwa la Sahara, Amerika Kusini na Carribea , kusini mwa Asia, mashariki mwa Asia na Pasifiki.

Kwa mujibu wa takwimu za UNICEF, Jamhuri ya Afrika ya Kati ina idadi kubwa ya ndoa za utotoni miongoni mwa wavulana ikiwa ni asilimia 28 ikifuatiwa na Nicaragua yenye asilimia 19 na Madagascariliyo na asilimia 13.

Hatahivyo, watoto walioko hatarini zaidi kuolewa mapema wanatoka katika kaya maskini, wanaishi vijijini na wana viwango vya chini vya elimu.

Unaweza kusoma ripoti kamili katika tovuti ya UNICEF www.unicef.org

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *