Migne ataja kikosi cha Harambee Stars kuelekea fainali ya AFCON

Spread the love

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Sébastian Migné  amekitaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kuelekea fainali ya mataifa bingwa barani Afrika nchini Misri.

Michuano ya AFCON itaanza tarehe 21 mwezi Juni, na Kenya imepangwa katika kundi moja na Algeria, Senegal na Tanzania.

Kenya ambayo imerejea katika michuano hiyo baada ya miaka 15 itaanza kampeni yake dhidi ya Algeria tarehe 23 mwezi Juni.

Harambee Stars ipo nchini Ufaransa inakoendelea na maandalizi kuelekea katika michuano hiyo.

Kikosi kamili:

Makipa Patrick Matasi, John Oyemba, Faruk Shikalo

Mabeki Philemon Otieno, Abud Omar, Bernard Ochieng, Musa Mohammed, Joash Onyango, Joseph Okumu, David Owino, Eric Ouma

Viungo wa Kati Victor Wanyama, Dennis Odhiambo, Erick Johanna, Ayub Timbe, Francis Kahata, Ismael Gonzalez, Ovella Ochieng, Paul Were, Johanna Omollo

Washambuliaji Masud Juma, Michael Olunga, John Avire

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *