Juventus yajipanga kumng’oa Pogba Old Trafford

Kiungo wa Manchester United Paul Pogba

Spread the love

Juventus ya Italia imeripotiwa akuwa pia inawania saini ya kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba.

Mchezaji huyom wa Manchester United pia anawaniwa na na Real Madrid ya Uhispania ambayo kocha wake Zinedine Zidane anawania kwa udi na uvumba saini ya mchezaji huyo.

Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo Fabio Paratici amesema amekutana na maofisa wa Manchester United ili kutathimini uhamisho wa mchezaji huyo ambaye alijiunga na United Juni 2016 akitokea Juventus kwa ada ya Pauni milioni 89.

Tayari Pogba ameonyesha tamaa ya kutaka kuondoka klabuni hapo lakini Kocha Ole Guna Sosha amesiisitiza kuwa mshindi huyo wa kombe la dunia yu sehemu ya mipango yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *