Mbappe haondoki PSG

Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe

Spread the love

Rais wa klabu ya PSG ya Ufaransa Nasser Al-Khelaifi amefichua kuwa ana uhakika wa aislimia 200 mshambuliaji Kylian Mbappe atasalia katika klabu hiyo msimu ujao.

Nyota huyo amekuwa akihusishwa kuihama PSG aliyojiunga nayo kwa mkataba wa kudumu msimu aliopita akitokea Monaco pia ya Ufaransa.

Msimu uliopita Mbappe alifunga mabao 39 katika mechi 43 alizocheza katika mashindano yote.

Akizungumza na jarida la France Football Khelaifi amesema anataka kuona wachezaji wa PSG wakijisikia fahari kuvaa jezi ya klabu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *