Chanjo ya Ebola kuanza kutolewa nchini Uganda

Maafisa wa WHO wakizungumza na maafisa wa afya katika hospitali ya Bwera karibu na mpaka wa Uganda na DRC, Juni 12, 2019. REUTERS/Samuel Mambo

Spread the love

Maafisa wa afya nchini Uganda wamepata idhini kutoka kwa Shirika la afya duniani WHO kuanza kutoa chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Hii ni baada ya watu wawili kupoteza maisha katika Wilaya ya Kasese Magharibi mwa nchi hiyo wiki iliyopita.

Watu hao walipoteza maisha ni mtoto wa miaka mitano na bibi yake, waliokuwa wamevuka mpaka kutoka DRC na kuingia nchini Uganda.

Tayari watu waliokutana na watu hao walioambukizwa Ebola wametengwa na kupewa chanjo hiyo ili kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo nje ya wilaya ya Kasese.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom ametembelea Mashariki mwa DRC na Uganda kujionea jitihada za kupambana na ugonjwa huo hatari.

Maambukizi ya Ebola yalianza kushuhudiwa mwezi Agosti mwaka uliopita Wilayani Beni na Ituri mashariki mwa DRC na kusababisha watu 1,400 kupoteza maisha na wengine zaidi ya 2,000 kuambukiza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *