Fatuma Samoura akitwa kusimamia shirikisho la soka Afrika CAF

Katibu Mkuu wa Fifa, Fatuma Samoura katika moja ya mikutano ya shirikisho hilo

Spread the love

Shirikisho la kandanda duniani FIFA na shirikisho la soka barani Afrika CAF zimefikia makubaliano ya kumteua Katibu Mkuu wa Fifa Fatuma Samoura kuwa mjumbe maalumu wa CAF katika uongozi wa soka.

Ikiwa uamuzi huo utaidhisnishwa Samoura ataanza rasmi kazi hiyo Agosti mosi na atahudumu kwa kipindi cha miezi sita.

Hatua hiyo inakuja katika kipindi ambacho CAF inakabiliwa na tuhuma za ukosefu wa maadili baada ya rais wa shirikisho hilo Ahmad Ahmad kuhojiwa na mamlaka za usalama nchini Ufaransa.

Vyanzo vya CAF vinasema ikiwa ataidhinishwa atalazimika kuachia baadhi ya majukumu yake ya kiutendaji katika Fifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *