Mamilioni yachangwa kuisaidia Taifa Stars

Makamu wa rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

Serikali ya Tanzania leo imefanya harambee ya kuichangia timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambayo iko nchini Misri kushiriki fainali za Afrika.

Hafla hiyo imefanyika katika hotel ya Serena na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ambapo mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Tanzania, samia Suluhu Hassan amenunua jezi ya timu hiyo kwa shilingi milioni tano huku wa ziri wa Habari Harrison Mwakyembe akinunua kwa shilingi milioni moja.

Mamilioni ya fedha yamechangwa na kampuni na taasisi mbalimbali huku mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiahidi kutoka eneo la uwanja wa hekari 15 kwa shirikisho la soka Tanzaniam TFF kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha soka.

Makamu wa rais amewataka watanzania kuisapoti kwa hali na mali timu hiyo wakati wote itakapokuwa ikishiriki.

Huko Burundi Shirikisho la Soka limeahidi kutoa Faranga za Burundi milioni 150 karibu dola 7000 ikiwa Burundi itaishinda Nigeria katika mchezo wa Afcon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *