Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania watoa taarifa ya kiusalama, serikali yasema watu watulie

Nembo ya serikali ya Marekani tz.usembassy.gov

Spread the love

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umetoa taarifa ya kiusalama katika maeneo yanayotembelewa na wageni katika jiji la kibiashara la nchi hiyo la  Dar es salaam.

Katika taarifa iliyotolewa kupitia tovuti ya Ubalozi huo, imeeleza kuwa kuna uvumi huenda mashambulizi hayo yakalenga mtaa wa kifahari wa Masaki, Hoteli ya Serena, Slipway na maeneo ya Msasani.

Hata hivyo, Ubalozi unasema hauna ushahidi wa kutokea kwa mashambulizi hayo, lakini unatoa wito wa watu kuwa makini na kuepuka mikusanyiko wa watu wengi.

Mkuu wa jeshi la Polisi nchini humo Simon Sirro amesema anafahamu kuhusu uvumi huo na maafisa wa usalama wanazifanyia kazi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameambia watu kwa njia ya video kuwa watulie vyombo vya usalama vya Tanzania zinafanya kazi kikamilifu na kuwataka wananchi kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao.

Tanzania haijawahi kulengwa na visa vya mashambulizi katika miaka ya hivi karibuni, isipokuwa mwaka 1998, wakati magaidi wa al-Qaeda waliposhambulia Ubalozi wa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 11.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *