Nigeria, Cameroon zafuzu hatua ya 16 bora, fainali za kombe la dunia za wanawake

Picha tofautio zikionyesha wachezaji wa timu za taifa za Nigeria na Cameroon africa news

Spread the love

Nigeria na Cameroon zimefuzu hatua ya 16 bora ya fainali za kombe la dunia za wanawake zinazoendelea nchini Ufaransa.

Cameroon imepata tiketi hiyo baada ya kushinda mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya NewsZealand kwa mabao mawili kwa bila wakatyi Nigeria ilikuwa ikisubiri matokeo ya Thailand ambayo ilitandikwa mabao 2-0 kwa Chile na hivyo kuipa upenyo Nigeria wa kufuzu hatua hiyo.

Hii ni mara ya kwanza kwa mataifa ya Afrika kufuzu hatua ya mtoano ya fainali za kombe la dunia kwa wanawake.

Afrika Kusini ni wawakilishi pekee wa Afrika walioshindw akufua dafu katika fainali hizo baada ya kufungwa michezo yote ya hatua ya makundi.

Nigeria na Cameroon sasa zinaungana na mataifa mengine ikiwemo Uingereza, Chilem Marekani, Australia, Italia, Brazil kufuzu hatua ya 16 bora.

Fainali hizo zilizoanza Juni 7 zitafikia tamati Julai 7 kwa mchezo wa fainali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *