Afya ya mshambuliaji wa Nigeria yaendelea kuimarika

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria Samuel Kalu goal.com

Spread the love

Afya ya Samuel Kalu, mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria inaendelea kuimarika, baada ya kuzirai wakati akifanya mazoezi nchini Misri.

Hii ilitokana na joto kali linaloshuhudiwa jijini Cairo, na watalaam wa afya wamesema kuwa alikosa maji ya kutosha mwilini.

Taarifa kutoka Shirikisho la soka nchini Misri, limesema kuwa Kalu, anayechezea klabu ya Bordeaux nchini Ufaransa, anaendelea vema na anaweza kucheza siku ya Jumapili, wakati nchi yake itakapomenyana na Burundi.

Hii ni mara ya kwanza mashindano haya yanachezwa katika majira ya joto, mwezi Juni na Julai nchini Misri, na hali ya joto inatarajiwa kupanda kati ya nyuzi joto 35 hadi 38.

Wachezaji wanaoshiriki katika michuano hii, wanatarajiwa na mapumziko ya dakika tatu inapotimia dakika ya 30 na 70 ili kunywa maji, kabla ya kuendelea na mchezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *