Chelsea yagangamala kwa Mateo Kovacic

Mateo Kovacic akiwa na ubingwa wa Europa msimu ulipita

Spread the love

Mabingwa wa Europa League, Chelsea wanagangamala kutaka kumsajili mojwa kwa moja kiungo Mateo Kovacic.

Mchezaji huyo yuko kwa mkopo katika klabu ya Chelsea aliyojiunga nayo msimu uliopita akitokea Real Madrid ya Uhispania.

Msimu uliopita mchezaji huyo wa kimataifa wa croatia alicheza mechi 32 katika kikosi cha chelsea na kufanikiwa kushinda taji la Europa kwa kuifunga Arsenal katika mchezo wa fainali.

Chelsea inasuka kikosi chake huku ripoti zikisema hivi karibuni itamtangaza Frank Lampard kuwa meneja wake mpya kwa mkataba wa miaka mitatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *