Misri,Nigeria za kwanza kufuzu 16 bora fainali za AFCON

Mohammed Salah akifunga bao la pili kwa Misri katika mchezo wa AFCON dhidi ya DRC

Spread the love

Mataifa ya Misri na Nigeria yamekuwa ya kwanza kufuzu hatua ya 16 ya michuano ya mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Misri.

Nigeria ilikuwa ya kwanza kufuzu hatua hiyo baada ya kuishinda Guinea kwa bao 1-0 katika mchezo wa kundi B na kufikisha alama sita.

Jana usiku pia Misri ilikata tiketi hiyo baada ya kuishinda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mabao 2-0 yaliyofungwa na El Mohammad na Mohammed Salah kipindi cha kwanza cha mchezo.

Misri ina alama sita ikisaliwa na mchezo mmoja dhidi ya Ugandna huku DRC ikingoja kukamilisha ratiba dhidi ya Zimbabwe kwa kuwa haina nafasi ya kufuzu hatua ya 16.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *