UN:Kauli za chuki sio uhuru wa kuongea, ni ubaguzi

Katibu Mkuu ameyasema hayo akizungumza katika mkutamo wa Baraza Kuu kuhusu kukabiliana na chuki dhidi ya Wayahudi na mifumo mingine ya ubaguzi wa rangi na chuki ikiwa ni pamoja na changamoto za kuelimisha kuhusu kuvumiliana na kuheshimiana katika zama hizi za kidijitali. Amesema kwa mujibu wa utafiti uliotolewa mwezi uliopita katika ripoti ya chuo kikuu cha Tel Aviv idadi ya matukio ya kikatili ya chuki dhidi ya Wayahudi yameongezeka kwa asilimia 13 mwaka 2018 ikilinganishwa na mwaka 2017. “Marekani, Ulaya na kwengineno mashambulizi dhidi ya Masinagogi, mkaburi na watu binafsi yameendelea kuwafanya Wayahudi kuwa na hofu kubwa. Katika enzi hizi chuki za zamani zinaonekana kushika usukani, na zaidi ya hapo kutovumiliana imekuwa ni jinamizi linaloongozwa na watu wengi” Hali halisi ya chuki Guterres ameongeza kuwa katika miezi ya karibuni katika sehemu mbalimbali duniani mbali ya mashambulizi kwenye Masinagogi tumeshuhudia mauaji misikitini na mashambulizi ya mabomu makanisani. Wahamiaji na wakimbizi wanaendelea kukabiliwa na upinzani na ukatili, wafuasi wa itikadi za watu weupe ndio kuonekana wa maana kuliko wengine zinaongezeka na sera za kinazi zinajipenyeza kwenye masuala ya uchaguzi na kuonyesha ujumbe wa kibaguzi. Katibu Mkuu amesema na katika zama hizo za kidijitali kuna wimbi kubwa na mabalozi wa kusambaza chuki kwenye majukwaa mapya ambayo watu wenye itikadi Kali wanaweza kukutana na kuchagizana. Picha na UN

Spread the love

Chuki dhidi ya Wayahudi bado ipo na ni moto unaoendelea kuwaka bila kuwepo dalili zinazoonekana za kuuzima, ameonya leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres .

Katibu Mkuu ameyasema hayo akizungumza katika mkutamo wa Baraza Kuu kuhusu kukabiliana na chuki dhidi ya Wayahudi na mifumo mingine ya ubaguzi wa rangi na chuki ikiwa ni pamoja na changamoto za kuelimisha kuhusu kuvumiliana na kuheshimiana katika zama hizi za kidijitali.

Amesema kwa mujibu wa utafiti uliotolewa mwezi uliopita katika ripoti ya chuo kikuu cha Tel Aviv idadi ya matukio ya kikatili ya chuki dhidi ya Wayahudi yameongezeka kwa asilimia 13 mwaka 2018 ikilinganishwa na mwaka 2017.

“Marekani, Ulaya na kwengineno mashambulizi dhidi ya Masinagogi, mkaburi na watu binafsi yameendelea kuwafanya Wayahudi kuwa na hofu kubwa. Katika enzi hizi chuki za zamani zinaonekana kushika usukani, na zaidi ya hapo kutovumiliana imekuwa ni jinamizi linaloongozwa na watu wengi”

Hali halisi ya chuki

Guterres ameongeza kuwa katika miezi ya karibuni katika sehemu mbalimbali duniani mbali ya mashambulizi kwenye Masinagogi tumeshuhudia mauaji misikitini na mashambulizi ya mabomu makanisani.

Wahamiaji na wakimbizi wanaendelea kukabiliwa na upinzani na ukatili, wafuasi wa itikadi za watu weupe ndio kuonekana wa maana kuliko wengine zinaongezeka na sera za kinazi zinajipenyeza kwenye masuala ya uchaguzi na kuonyesha ujumbe wa kibaguzi.

Katibu Mkuu amesema na katika zama hizo za kidijitali kuna wimbi kubwa na mabalozi wa kusambaza chuki kwenye majukwaa mapya ambayo watu wenye itikadi Kali wanaweza kukutana na kuchagizana.

Chanzo:UN Kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *