ICC: Hukumu dhidi ya Bosco Ntaganda kutolewa Jumatatu hii

Mbabe wa kivita Bosco Ntaganda, anahukumiwa leo na mahakama ya kimataifa inayoshughulikia makosa ya uhalifu, ICC

Spread the love

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, inatarajia kutoa leo Jumatatu Julai 8 hukumu dhidi ya kiongozi wa zamani wa kivita nchini DRC Bosco Ntaganda.

Majaji wanatarajia kuamua ikiwa kiongozi huyo wa zamani wa kivit ana hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa mwaka 2002 na 2003 katika Jimbo la Ituri, mashariki mwa DRC.

Je, Bosco Ntaganda ni mpiganaji jasiri, aliyejihusisha na kuheshimu sheria za vita kama vile watetezi wake wanavyosema? Au ni Terminator (Mkomeshaji) kama unavyomuita upande wa mashitaka?

Ntaganda atasimama mbele ya majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita, ICC, kujibu mashtaka ya tuhuma za kusimamia mauji na kuwatumia watoto kwenye jeshi lake la waasi.

Ntaganda anakabiliwa na makosa 13 ya uhalifu wa kivita na matano ya uhalifu dhidi ya binadamu, kwa ajili ya jukumu lake kwenye mgogoro wa kikatili wa vita ya wenyewe kwa wenyewe katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Ntaganda ambaye ana asili ya Rwanda, mnamo mwezi Septemba 2015 alikanusha kuhusika na uhalifu huo mwanzoni mwa kesi yake mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.

Waendesha mashitaka katika mahakama ya ICC iliyoko mjini the Hague, wanasema jeshi lake la waasi kati ya mwaka 2002 na 2003 lilifanya utawala wa hofu katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Ituri, na kusababisha unyanyasaji wa kutisha dhidi ya wenyeji.

Ntaganda alipanga operesheni za jeshi lake la Patriotic Forces for the Liberation of Congo (FPLC), akiwatumia watoto kama askari na kuwalazimisha wanawake katika utumwa wa ngono, wakati akiwashambulia raia kwa misingi ya kikabila.

Mahakama ya ICC imesema hukumu dhidi ya kongozi huyo wa zamani wa waasi itatolewa leo Jumatau Julai 8.

Chanzo:RFI Kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *