Rais Magufuli aombolewa msiba wa wafanyakazi wa Azam Media

Rais John Magufuli

Spread the love

Rais John Magufuli ametoa salamu za rambirambi kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea mkoani Singida na kusababisha vifo vya watu watano wakiwemo wafanyakazi watano wa Kampuni ya Azam Media.

Katika taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano ya rais iliyotolewa na Ikulu, Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na tukio hilo na kutoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa makini wawapo barabarani.

Wakati huohuo Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Azam Media Tido Muhando amesema kampuni hiyo imepoteza nguvu kazi kubwa.

“Maiti zipo katika hospitali ya Igunga na majeruhi wapo katika hospitali ya Iramba Mkoani Singida.

Kufuatia msiba huo, Mhando amesema vituo vya luninga vya Azam vitabadilisha utaratibu wa vipindi kutokana na shughuli za maembolezo na mazishi kwa wapendwa waliopoteza maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *