Marekani yaanzisha uchunguzi kuhusu mpango wa Ufaransa kutoza kodi kampuni za teknolojia

Kampuni za Marekani ambazo huenda zikaathirika na mpango wa Ufaransa wa kuongeza kodi kwa kampuni za teknolojia za Marekani.

Spread the love

Serikali ya Marekani imeanzisha uchunguzi kuhusu mpango wa Ufaransa kuanza kutoza kodi kampuni za teknolojia.

Marekani kupitia mwakilishi wake wa masuala ya biashara Robert Lighthizer inasema mpango wa Ufaransa hauna tija na unazilenga kampuni za teknolojia za Marekani.

Ikiwa Ufaransa itaendelea na mpango wake itathiri ukusanyaji wa mapato kwa mwaka, karibu dola za Marekani milioni 844.

Marekani inasema kampuni zinazolengwa ni pamoja na Alphabet Inc’s Google, Apple Inc, Facebook Inc na Amazon.

Hata hivyo kampuni inayojishughulisha na ushauri wa kiteknolojia ya ITI imeitaka serikali ya Marekani kutolipiza kisasi kwa kutoza ushuru kampuni za teknolojia za Ufaransa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *