Mtanzania auawa katika shambulio la Al Shabaab nchini Somalia

Al Shabaab ilikuwa ikidhibiti maeneo kadhaa ya Somalia kabla ya kurudishwa nyuma na majeshi ya Afrika

Spread the love

Shambulio lililotekelezwa na kundi la Al Shabaab katika mji wa Kismayu nchini Somalia limesababisha vifo vya watu ishirini na sita akiwemo Mtanzania.

Mtanzania aliyeuawa katika shambulio hilo ni Mahdi Abdullahi Nur ambaye alikuwa mkurugenzi wa Hoteli ya Paradise Holiday Resort iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.

Watu wengine waliopoteza maisha ni kutoka mataifa ya Kenya, Marekani na Canada.

Inaelezwa shambulio hilo limetokea katika hoteli moja ya kifahari katika mji wa Kismayu.

Kundi la Al Shabaab limekuwa likitekeleza mauaji nchini Somalia, taifa ambalo limekosa serikali imara tangu kupinduliwa kwa rais Siad Barre mwanzoni mwa miaka ya tisini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *