Mechi ya kusaka mshindi wa tatu Afcon kucheza kesho Julai 17

Uwanja wa Al Salaam utakaotumiwa kwa mchezo baina ya Nigeria na Tunisia. Picha na Goal.com

Spread the love

Timu za Taifa za Nigeria na Tunisia kesho zitashuka uwanjani kuumana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu katika mfululizo wa fainali za Afrika.

Mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Al Salaam na itakuwa mara ya tano kwa timu hizo kukutana katika michuano ya Afrika.

Nigeria ilishindwa mabao 2-1 na Algeria katika mchezo wa nusu fainali ilihali Tunisia ilichapwa bao 1-0 na Senegal katika hatua ya nusu fainali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *