Wakala akanusha Bale kuhusishwa kujiunga na Spurs

Nyota wa Real Madrid, Gareth Bale

Spread the love

Jonathan Barnett, wakala wa mshambuliaji wa Real Madrid amekanusha mchezaji huyo kuwa mbioni kujiunga na Tottenham Hotspurs.

Bale alikuwa mchezaji wa Spurs kabla ya kujiunga na Real Madrid mwaka 2013, usajili uliovunja rekodi ya uhamisho wa wachezaji duniani wakati huo.

Barnatt amesema hana muda wa kutoa maoni kuhusu taarifa za kipuuzi zinazomhusisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales kujiunga na Spurs.

Bale anakabiliwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha Madrid na anaonekana hayumo kwenye mipango ya meneja wa klabu hiyo Zinedine Zidane.

Real Madrid imetumia zaidi ya Euro milioni 270 katika majira haya ya joto kuwasajili Eder Militao, Eden Hazard, Luka Jovic na Ferland Mendy.

Tetesi zinasema Spurs iko tayari kulipa Euro milioni 60 ili kumsajili Bale.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *