KCCA yashinda taji la Kagame Cup

Wachezaji wa KCCA wakishangilia baada ya kuibuka mabingwa wa michuano ya kombe la Kagame

Spread the love

Mabingwa wa soka nchini Uganda, KCCA imeshinda kwa mara ya kwanza taji la michuano ya Kombe la Kagame hapo jana baada ya kusihinda Azam FC ya Tanzania kwa bao 1-0.

Azam ndio waliokuwa mabingwa watetezi wa taji hilo, wakishinda mara mbili mfululizo.

Mwaka 2015 Azam iliishinda Gor Mahia mabao 2-0 na mwaka jana iliishinda Simba mabao 2-1 katika mchezo wa fainali.

Kwa kunyakua taji hilo KCCA ambayo itawakilisha Uganda katika michuano ya klabu bingwa Afrika inaingia katika orodha ya timu za Uganda zilizoshinda taji hilo, nyingine zikiwa ni SC Villa na Polisi FC.

Hii ni mara ya pili kwa KCCA kushinda taji hilo, mara ya mwisho walishinda mwaka 1978.

KCCA imetwaa taji hilo licha ya kuwakosa wachezaji wake mashuhuri kama Allan Kyambade, Patrick Kaddu na Timothy Awamy ambao walikuwa kwenye kikosi cha Uganda kilichoshiriki michuano ya mataifa ya Afrika nchini Misri.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *