Mashami:Rwanda inaweza kufuzu fainali za Afrika 2021

Kocha wa Timu ya Taifa ya Rwanda, Vincent Mashami

Spread the love

Kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda, Vincent mashami amesema kwamba timu yake ina nafasi ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2021.

Droo ya makundi ya michuano hiyo ilitangazwa wiki iliyopita huku Rwanda ikipangwa sambamba na Cameroon, Cape Verde na Msumbiji. Timu mbili kwa kila kundi zitafuzu kucheza fainali hizo zitakazofanyika nchini Cameroon

Mashami hata hivyo amenukuliwa na gazeti la New Times kuwa timu yake inapaswa kujiandaa kikamilifu ili kufanikisha adhma ya kufuzu fainali hizo kwa mara ya pili.

Rwanda imeshiriki mara moja fainali za Afrika, mwaka 2004 zilipofanyika nchini Tunisia.

Rwanda inashikilia nafasi ya 136 katika orodha ya ubora wa viwango vya FIFA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *