Shirikisho la kandanda nchini Kenya lapata Kaimu Mkurugenzi mpya

Nick Mwendwa akiwa na Barry Otieno. Picha kwa hisani ya Daily Nation

Spread the love

Shirikisho la kandanda nchini Kenya limetanza kumpandisha ngazi mkuu wa kitengo cha mawasiliano Barry Otieno kuwa Kaimu mtendaji mkuu wa shirikisho hilo.

Hatua hiyo inachukuliwa kwa lengo la kuimarisha taswira ya taasisi hiyo kutokana na mfululizo wa shutuma na tuhuma mbalimbali.

Aliyekuwa mkurugenzi wa FKF Robert Muthon alilazimika kukaa pembeni kwa tuhumza za kusaidia uhamisho wa mchezaji wa Sofapaka Joseph Avire.

Ijumaa iliyopita FKF ilitangaza kuanzisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili Muthoni.

Rais wa FKF Nick Mwendwa anakabiliwa na shinikizo la kutuliza hali ya hewa ndani ya shirikisho la kandanda nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *