Mooketsi Kgotlele, katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini Botswana ahukumiwa maisha kujihusisha na soka

Shirikisho la kandanda duniani Fifa, limemfungia maisha katibu mkuu wa shirikisho la kandanda nchini Botswana

Spread the love

Shirikisho la kandanda duniani Fifa limetangaza kumfungia Mooketsi Kgotlele maisha kujihusisha na soka.

Kgotlele alikuwa katibu mkuu wa shirikisho la kandanda nchini Botswana BFF na anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ya rushwa.

Kamati ya maadili ya Fifa imempata na hatia ya kupokea rushwa ili kufanya udanganyifu katika mechi za kimataifa.

Kufuatia uamuzi huo wa Fifa, Kgotlele hataruhusiwa kujihusisha na shughuli yoyote ya utawala na michezo na pia amepigwa faini ya dola za Marekani 51,000

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *