Mussa Bility akimbilia CAS, kuishtaki FIFA, CAF

Mussa Bility, Mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF

Spread the love

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la kandanda Afrika CAF, Mussa Bility amesema atafungua shauri katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo akieleza kutoridhishwa na makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirikisho la kandanda duniani FIFA NA shirikisho la kandanda barani Afrika CAF.

Katika taarifa yake Bility anafungua shauri hilo akiitaka CAS itamke kuwa makubaliano hayo ni batili na hayakubaliki.

Makubaliano baina ya CAF na Fifa yanasema katibu mkuu wa Fifa, Fatma Samoura kuwa mjumbe maalumu wa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF.

Bility, rais wa zamani wa chama cha soka nchini Liberia anasema anaamini CAS “iseme hatua hiyo inaweza kupelekea mkakati wa CAF kuwekwa mfukoni na Fifa”

Hata hivyo wakati mpango huo ukiafikiwa, rais wa Fifam Gian Infantino alisema anaamini hatua hiyo itasaidia ukuaji wa soka barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *