Victor Matine ateuliwa kuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya msumbiji

Victor Matine, kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Msumbiji

Spread the love

Victor Matine ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa Timu ya Taifa ya Msumbiji, akichukua nafasi ya Abel Xavier ambaye mkataba wake umemalizika.

Mkataba wa Xavier hautaongezwa kutokana na kushindwa kuiwezesha Msumbiji kushindwa kushiriki fainali za Afrika.

Matine alikuwa msaidizi wa Xavier na kibarua kizito kinachomkabili ni kuiwezesha Msumbiji kushiriki mechi za mchujo wa kufuzu kwa fainali za Afrika na zile za CHAN.

Matine atasaidiwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Msumbiji Nelihno.

Alberto Simango, Mkuu wa Shirikisho la kandanda nchini Msumbiji anasema mikakati ya shirikisho hilo ni kuhakikisha Msumbiji inafuzu kucheza fainali zijazo za Afrika.

Msumbiji itachuana na Madagascar katika mchezo wa kufuzu kwa michuano ya CHAN mwishoni mwa wiki hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *