Zidane akanusha ripoti kuwa anamdharau Gareth Bale

Zinadine Zidane akiwa na wachezaji wake mazoezini

Spread the love

Meneja wa Real Madridm Zinedine Zidane amekanusha madai kuwa hamheshimu winga Gareth Bale na kusema mchezaji huyo alikataa kuingia kipindi cha pili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Bayern Munich.

Zidane awali alitangaza kuwa Bale yu karibu kuihama Real Madrid, uhamisho aliosema utakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.

Bale alijunga na Real Madrid mwaka 2013 na amekuwa katika sintofahamu na meneja wake kutokana na kutopata nafasi ya kutosha uwanjani.

“Sijaonyesha kutomheshimu Bale nilichosema ni kwamba klabu inafanya utaratibu wa kufanikisha uhamisho wake”amesema Zizzou, mshindi mara tatu wa taji la klabu bingwa Ulaya.

Bale anahusishwa  kujiunga na klabu moja inayoshiriki ligi kuu ya Uchina

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *